UNAPENDA MAGARI? SUBSCRIBE NOW

Thursday, October 5, 2017

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE - NAFASI 56

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE

Mkurugenzi Mtendaji (W)Makete kupitia kibali cha ajira mbadala kilichotolewa na
Katibu Mkuu - Utumishi Kumb. Na. CFC 26/205/01"FF" /91 anapenda
kuwatangazia Wananchi wote wenye sifa za kuajiriwa kuleta maombi yao yao kwa nafasi zifuatazo

MTENDAJI WA KIJIJI III - NAFASI 56
1.1. MAJUKUMUYA KAZI
(i) Kuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
(ii) Kusimamia ulinzi na usalama.
(iii)Kusimamia utawala bora katika Kijiji
(iv)Kuwa katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
(v) Kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu zinazoongoza Serikali ya kijiji
(vi)Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za
Kijiji.

NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara ya TGS B kwa mwezi.


SIFA ZAMWOMBAJI
Mhitimu wa kidato cha nne au sita waliohitimu mafunzo ya cheti katika moja ya
fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa fedha, Maendeleo ya
Jamii au Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikari za Mitaa Hombolo, Dodoma
au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

MASHARTIYA UJUMLA
(i)Mwombaji wote wawe ni raia wa Tanzania
(ii)Waombaji wote waambatanishe nakala ya cheti cha kuzaliwa
(iii)Waombaji wote waambatanishe na maelezo binafsi (CV)
(iv)Waombaji waambatanishe picha 1 "Passport Size" ya hivi karibuni na
nakala za vyeti halisi.
(v)Transcript "Testmonials" na "Provisional Results" au Statement of Results
havitakubaliwa.
(vi)Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na usiopungua miaka 18.
(vii) Kwa waombaji ambao walishatuma maombi yao kupitia Tangazo la nafasi
sita za Watendaji wa Vijiji III la tarehe 28/08/2017 wasitume maombi kwa
kuwa barua zao zipo na zitatumika kwa ajili ya maombi ya kibali kilichotangazwa kupitia Tangazo hili.

6. MAOMBI YATUMWE KWA:

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya ya Makete,
S.L.P.6,
Makete.

MWISHO WA KULETA MAOMBI
Maombi yawasilishwe kabla au mnamo tare he 17/10/2017 saa 9:30 Alasiri.
Maombi yatakayowasilishwa baada ya tare he na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.
logoblog

Thanks for reading TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE - NAFASI 56

Previous
« Prev Post