UNAPENDA MAGARI? SUBSCRIBE NOW

Tuesday, September 26, 2017

NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA TANZANIA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/ J/46 25 Septemba 2017

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Shirika la
Masoko Kariakoo (KARIAKOO MARKETS CORPORATION) anakaribisha maombi ya
kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 4 kama
inavyoonekana katika tangazo hili.

1.0 MENEJA WA FEDHA

1.1MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuwa mshauri Mkuu wa Meneja Mkuu kuhusu masuala ya fedha za Shirika
ii. Kuwasimamia na kuwaongoza wafanyakazi wote wa idara ya uhasibu
iii. Kuandaa na kuweka sawa mfumo wa Hesabu za Shirika na kuhakikisha
kuwa malengo ya ukusanyaji yanafikiwa
iv. Kuhakikisha kuwa vitabu vya fedha vinaandaliwa na ukaguzi wa nje
unafanyika kulingana na kanuni na miongozo ya shirika.
v. Kuweka muundo sahihi wa fedha kwa ajili ya Shirika na kuhakikisha
upatikanaji na usambazaji wa fedha unafaa.
vi. Kuhakikisha kuwa kanuni za fedha zinafuatwa
vii. Kutayarisha bajeti ya mwaka pamoja na mifumo ya udhibiti wa bajeti kama
itakavyoelekezwa na Meneja Mkuu au Bodi ya Wakurugenzi.
viii. Kufanya kazi nyingine kama atakavyoagizwa na Meneja Mkuu

1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Mwombaji awe na cheti cha CPA(T), awe amesajiliwa na NBAA kama
Mhasibu aliyethibitishwa, Shahada ya Uzamili (MBA, Msc Finance).
 Pamoja na uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi (10)
1.1.3 MENEJA BIASHARA NA MIPANGO

1.1.4 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuendesha mfumo sahihi wa mipango kwa ajili ya Shirika zima na
utayarishaji mipango inayotumiwa na Idara zote za Shirika.
ii. Kuratibu utayarishaji mipango wa muda mfupi na mrefu na kutoa msaada
wa kiufundi katika mipango yote inapohitajika
iii. Kusimamia uendeshaji wa shughuli zote zinazoleta pato kibiashara kwa
Shirika

iv. Kuelekeza na kusimamia watumishi wote katika idara ya Biashara
v. Kutoa taarifa za kibiashara kwa Meneja Mkuu kuhusu mwenendo mzima wa
Biashara katika Shirika.
vi. Kutoa taarifa za kibiashara kwa Meneja Mkuu kuhusu mwenendo mzima wa
Biashara katika Shirika.
vii. Kufanya kazi yoyote atakayopangiwa na Meneja Mkuu

1.1.5 SIFA ZA MWOMBAJI
 Mwombaji awe na shahada ya Uzamili ya Biashara au Uchumi kutoka
chuo Kikuu kinachotambulika na Serikali na Uzoefu wa kazi usiopungua
miaka kumi (10)

1.1.6 MENEJA RASILIMALI WATU NA UTAWALA

1.1.7 MAJUKUMU YA KAZI
i. Atamsaidia Meneja Mkuu katika masuala yote ya Rasilimali watu na Utawala
ii. Mratibu wa mikutano ya Shirika
iii. Utayarishaji wa Bajeti kwa kushirikiana na Meneja wa Fedha
iv. Kushauri juu ya kazi na taratibu za ajira katika Shirika
v. Kusimamia uwekaji wa kumbukumbu za watumishi wote wa Shirika
vi. Kusimamia viwango na taratibu za maslahi ya watumishi, likizo, fidia,
mafunzo, kupandishwa vyeo, nyongeza za mishahara na utunzaji wa
nyaraka mbalimbali za kuhakikisha kuwa vinafuatwa na kila Idara au
Vitengo katika Shirika.
vii. Kuhakikisha kuwa Kanuni za Utumishi, mifumo na miongozo mbalimbali ya
utawala inafuatwa.
viii. Kuhakikisha kuwa tathmini ya utendaji kazi (Performance Appraisal)
inafanyika kila mwaka.
ix. Kuhakikisha kuwa zoezi la kila mwaka la kupandisha watumishi vyeo,
mpango wa mafunzo, kuthibitisha watumishi kazini, ratiba za likizo n.k
vinatekelezwa ipasavyo.
x. Kutayarisha mpangilio wa elimu ya wafanyakazi.
xi. Kufanya kazi yoyote inayohusiana na Idara atakayopangiwa na Meneja
Mkuu.

1.1.8 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na shahada ya uzamili katika fani ya Menejimenti ya Rasilimali
watu, Uongozi na Utawala wa Umma au mwenye sifa zinazolingana na
hizo.
 Uzoefu wa kazi usiopungua miaka kumi (10)

1.1.9 MKUU WA KITENGO CHA UNUNUZI WA UGAVI

1.1.10 MAJUKUMU YA KAZI
Atakuwa Mshauri Mkuu wa Shirika kwenye masuala yote yanayohusu manunuzi
na uuzaji wa mali chakavu za Shirika kwa njia ya Zabuni au mnada, kwa mujibu
wa Sheria na Kanuni za Manunuzi ya Umma
i. Kuandaa na kutekeleza mpango wa manunuzi wa mwaka (Annual
Procurement Plan) wa Shirika.
ii. Kupanga na kusimamia manunuzi yote au uuzaji wa vifaa chakavu vya
Shirika kwa njia ya zabuni au mnada kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za
Manunuzi.
iii. Atakuwa katibu wa Bodi ya Zabuni Shirika.
iv. Kuandaa makabrasha ya zabuni (Tendering documents) na kuwapatia
wazabuni
v. Kuandaa na kutangaza matangazo ya zabuni
vi. Kuandaa mikataba ya zabuni
vii. Kuwapatia wazabuni walioshinda mikataba ya kazi
viii. Kuhifadhi na kutunza usalama wa taarifa zote zinazohusiana na manunuzi
na uuzaji wa mali za Shirika na kuzionesha taarifa hizo pale zinapohitajika.
ix. Kuhifadhi na kutunza kiusalama taarifa zote zinazohusiana na manunuzi na
uuzaji wa mali za Shirika na kuzionesa taarifa hizo pale zinapohitajika.
x. Kuhifadhi na kuitunza mikataba yote ya zabuni za Shirika
xi. Kuandaa taarifa za kila mwezi za utendaji wa zabuni wa Shirika na
kuziwasilisha kwenye bodi ya zabuni
xii. Kuratibu ufanyaji kazi wa Bodi ya Zabuni ya Shirika kwa mujibu wa Shirika.
xiii. Kuhakikisha kuwa kanuni na taratibu zote za stoo zinafuatwa
xiv. Kuhakikisha usalama unakuwepo kwenye mali yote iliyopo stoo/ghala
xv. Kusaidiana na Wakuu wa Idara na Vitengo kuratibu na kuweka
kumbukumbu za vifaa vilivyochakaa, thamani yake na vile ambavyo
havijachakaa.
xvi. Kuandaa taarifa mbalimbali za kitengo zinazohitajika na Menejimenti au
Mamlaka ya kurabitu manunuzi ya umma (PPRA)
1.1.11SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na Shahada au Stashahada ya juu ya “Materials Management” au sifa
zinazolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali. Awe pia
na cheti cha CPSP na amesajiliwa na PSPTB na ujuzi usiopungua miaka
saba (7).
 Shahada ya uzamili itakuwa ni sifa ya ziada.

MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya
kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya
kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Oktoba, 2017.
xii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA
xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa
Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz /
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya
Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment
Portal’)

MUHIMU: 

KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA
KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU.
ANUANI YA BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100
DAR ES SALAAM.
Katibu


Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
logoblog

Thanks for reading NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA AJIRA TANZANIA

Previous
« Prev Post