NAFASI 8 ZA KAZI: AGAPE ADVENTIST PRE & PRIMARY SCHOOL

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Shule ya Agape Adventist Pre & Primary School, inawatangazia nafasi za kazi kama ifuatavyo;

WALIMU NAFASI 4

i.MWALIMU WA SOMO LA KISWAHILI – NAFASI 1
SIFA:   Awe na uwezo mkubwa/amebobea kufundisha somo la Kiswahili kwa ufasaha
•Awe na diploma (stashahada) au shahada katika somo la Kiswahili na somo jingine la ziada.
•Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.

ii.MWALIMU WA DARASA LA KWANZA NA DARASA LA PILI – NAFASI 3
SIFA : Awe na  stashahada au shahada ya ualimu na uzoefu wa muda mrefu.
•Awe na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza na Kiswahili kwa ufasaha.
•Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha “kusoma”  kwa njia ya vitamkwa –Foni (phonics)
•Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha “kuandika” kwa ufasaha.
•Awe na uwezo mkubwa wa kufundisha matendo ya hisabati kwa ufasaha

MATRON – NAFASI 1
SIFA:Awe na umri wa miaka 40 au zaidi
•Awe amehitimu angalau elimu ya sekondari
•Awe amesomea taaluma ya lishe au uuguzi
•Awe na uzoefu wa muda mrefu katika taaluma yake
•Awe na uwezo wa kufundisha neno la Mungu na mwenye msimamo mzuri katika mambo ya kiroho
•Awe na uwezo wa kuongoza
•Mwenye uwezo wa kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza atapewa kipaumbele.

NESI (MUUGUZI) – NAFASI 1

SIFA : Awe na umri wa miaka 25 au zaidi na mwenye mapenzi na watoto.
•Awe na cheti katika mafunzo ya uuguzi.
•Awe na uzoefu usiopungua miaka 2
•Awe mtu anayeweza kujisimamia katika kazi yake.

MLEZI WA WATOTONAFASI 2

SIFA : Awe na elimu ya sekondari
•Awe na mapenzi kwa watoto
•Awe mchapa kazi, msafi na mwenye uwezo wa kujisimamia katika kazi
•Mwenye uzoefu wa malezi ya watoto atapewa kipaumbele.
Barua zifikishwe kwa:  i) Mkono ofisini Agape pre and Primary School  ii)  Anuani ya posta.
Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 7 /11/2016 saa 8:00 mchana.
Kumbuka kuandika namba ya simu kwenye barua yako.
Maombi yatumwe kwa:   MKUU WA SHULE
               AGAPE ADVENTIST PRE & PRIMARY SCHOOL
                P.O.BOX 751
                MOROGORO
Au tuma kwa E-mail: agapeadventist@gmail.com
============

Click HERE for more jobs.

============
Are you disappointed by fruitless job applications and never get shortlisted? The problem is not you, its your CV. This comes to an end, Now for outstanding CV and Jobs professional advice, contact Bright Professionals Tanzania  and grab your dream job. We  also prepare social science business researches  and proposals.
Email cv.bptz@gmail.com
Phone +255 678 226 793

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment "NAFASI 8 ZA KAZI: AGAPE ADVENTIST PRE & PRIMARY SCHOOL"

Back To Top