TCU: TAARIFA KWA UMMA

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
MGOGORO BAINA YA UONGOZI NA WANAFUNZI WA MWAKA
WA TATU WA SHAHADA YA UDAKTARI KATIKA CHUO KIKUU
KISHIRIKI CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI CHA MTAKATIFU
FRANCIS (SFUCHAS), IFAKARA
1. Tunapenda kuuarifu umma kwamba, Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya
na Sayansi Shirikishi cha Mtakatifu Francis ni miongoni mwa Vyuo
Vikuu vilivyosajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
2. Kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sura ya
346 ya Sheria za Tanzania, Tume ina mamlaka ya kusimamia na
kudhibiti ubora na usimamizi wa uendeshaji wa Vyuo Vikuu hapa
nchini.
3. Hivi karibuni Tume ilipokea taarifa ya kuwepo kwa mgogoro baina
ya Uongozi wa Chuo na Wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma
shahada ya udaktari wa binadamu (MD3). Kwa mujibu wa taarifa
hiyo, kiini cha mgogoro huo ni kuwepo kwa dosari katika matokeo
ya mitihani ya muhula wa tano (end of semester 5 examinations),
ambao hatimaye ulisababisha wanafunzi wote wa mwaka wa tatu
kufukuzwa chuoni.

4. Ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huo, Tume imechukua hatua
zifutazo:
a) Imewasiliana na Uongozi wa Chuo na kuuagiza stahiki kupitia
upya uamuzi wa kufukuza wanafunzi hao kwa kuzingatia sheria
zilizopo ili kutenda haki na kuondoa migogoro.
b) Imeunda Timu ya Wataalam kwenda kuchunguza kiini cha
mgogoro huo na kubainisha ukweli kuhusu tukio hili kwa lengo
la kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.
5. Kwa taarifa hii, Tume inawaomba wanafunzi wote wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Mt. Francis popote pale walipo, kuendelea kuwa
watulivu wakati huu ambapo suala lao linashughulikiwa na Chuo na
Tume.
Imetolewa na
PROF. ELEUTHER MWAGENI
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
31 Mei 2016
============

Avoid scams : NEVER pay to have your CV / Application pushed forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a SCAM.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment "TCU: TAARIFA KWA UMMA"

Back To Top