JISHINDIE ZAWADI YA GARI, CAMERA, SPEAKER NK KILA MWEZI, BONYEZA HAPA KUJISAJILI BURE KISHA FUATA MAELEKEZO

NACTE: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Tarehe 3 Juni 2016 ilikuwa siku ya mwisho ya kuwasilisha maombi ya udahili wa kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja unaoratibiwa na NACTE.
Baraza linapenda kuwaarifu waombaji udahili wa kozi tajwa hapo juu na umma kwa ujumla kuwa, kwa sasa maombi yote yaliyowasilisha mpaka tarehe 3 Juni 2016 saa sita usiku yameanza kuchambuliwa kwa ajili ya kuchagua waombaji wenye sifa stahiki. Zoezi la kuchambua waombaji udahili na hatimaye kuchagua waombaji wenye sifa stahiki na waombaji hao kuidhinishwa na mamlaka husika na kutangazwa litachukua muda wa wiki tatu hadi nne kuanzia tarehe 3 Juni, 2016.
Baraza linatambua uwepo wa waombaji wapya na baadhi ya waombaji walioshindwa kuwasilisha maombi yao kupitia mtandao ilipofika tarehe 3 Juni 2016. Waombaji wa namna hii na wengine wanaopenda kuwasilisha maombi yao kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja wanaombwa kuwa na subira mpaka hapo majina ya waombaji waliowasilisha maombi yao kabla ya kufungwa kwa mfumo watakapotangazwa.
Baada ya kutangazwa majina ya waombaji waliochaguliwa, Mfumo wa Udahili wa Pamoja utafunguliwa tena kwa ajili ya kujaza nafasi za udahili ambazo zitakuwa wazi na waombaji waliowasilisha maombi yao kuanzia tarehe 4 Machi, 2016 hadi tarehe 3 Juni 2016.
Baraza linatarajia kufungua tena Mfumo wa Udahili wa Pamoja kwa ajili ya kozi za Cheti, Diploma, Diploma ya juu na Shahada ya kwanza kati ya wiki ya mwisho ya mwezi wa sita, 2016  na wiki ya kwanza ya mwezi wa saba , 2016.

Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
NACTE
Tarehe: 7 Juni, 2016
===========
Follow us on Instagram

JISHINDIE ZAWADI YA GARI, CAMERA, SPEAKER NK KILA MWEZI, BONYEZA HAPA KUJISAJILI BURE KISHA FUATA MAELEKEZO

============

Avoid scams : NEVER pay to have your CV / Application pushed forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a SCAM.

============

Are you disappointed by fruitless job applications and never get shortlisted? The problem is not you, its your CV. This comes to an end, Now for outstanding CV and Jobs professional advice, contact Bright Professionals Tanzania and grab your dream job. We also prepare social science business researches and proposals.

Contact us via


Phone: 0678 226 793

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment "NACTE: TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGWA KWA MUDA WA KUPOKEA MAOMBI YA UDAHILI WA KOZI ZA CHETI, DIPLOMA, DIPLOMA YA JUU NA SHAHADA YA KWANZA KUPITIA MFUMO WA UDAHILI WA PAMOJA UNAORATIBIWA NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)"

Back To Top