NAFASI 632 ZA AJIRA SERIKALINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/102 
03 Februari, 2016

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 632 kwa ajili ya Wizara, Taasisi
zinazojitegemea na mamlaka za Serikali za Mitaa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za
vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango
hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za
kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
.

v. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
x. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 17 Februari, 2016
xi. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza..
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia
sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
ii. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (TO ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI
KWENYE SEHEMU YA ‘OTHER ATTACHEMENTS’.
iii. VYETI NA WASIFU (CV) VITAKAVYOTUMWA BILA BARUA YA MAOMBI
HAVITAFIKIRIWA.
iv. WAOMBAJI WANATAKIWA KUANDIKA MAJINA YA VYUO VYAO NA KOZI KWA
KIREFU (Eg. Bachelor of Science with Computer Science, University of Dar es
Salaam, na msiandike, BSc. Computer Science UDSM)
1.0AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 4
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
 Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
 Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
 Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo
kwa wataam wa mifugo na wafugaji.

 Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani
kwake na mkoani.
 Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
 Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya
mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
 Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama
katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
 Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
 Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
 Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa
malisho.
 Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
 Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
 Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na
mkuu wake wa kazi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo
(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa
inayolingana nayo.
1.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
2.0MTEKNOLIJIA WA SAMAKI DARAJA LA II (FISH TECHNOLOGISTS II) –
NAFASI 1
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutoa ushauri juu ya utayarishaji, utengenezaji, ukaushaji na uhifadhi wa samaki
na mazao yatokanayo na uvuvi.
 Kusimamia kushauri juu ya kanuni za uthibiti ubora wa Samaki na mazao yake
 Kutoa ushauri juu ya matumizi mbalimbali ya samaki kama chakula bora katika
Viwanda na maeneo mengine.
 Kudhibiti ubora wa samaki katika mialo.
 Kudhibiti usafi katika maeneo ya kupokelea samaki.
 Kukagua nyaraka mbalimbali zinazotakiwa kutunzwa melini na viwandani.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Chakula
(Food Science and Nutrition, Food Technology, Microbiology) kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.

2.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
3.0DAKTARI WA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY OFFICERS) – NAFASi 12
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutoa huduma za afya ya mifugo
 Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo katika eneo au sehemu alipo.
 Kutayarisha na kusimamia mipango ya kuzuia, kudhibiti na kutokomeza
magonjwa ya mifugo katika eneo lake.
 Kushiriki katika uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pori katika eneo lake.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Tiba ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari wa Mifugo nchini.
3.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
4.0 AFISA UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (LIVESTOCK RESEARCH OFFICER II) –
NAFASI 3
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kujifunza kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa mifugo/ndorobo
 Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Afisa Utafiti Mwandamizi.
 Kuandika na Kuweka kumbukumbu za utafiti.
 Kusaidia kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
 Kuandaa mapendekezo ya utafiti (Research Proposals) kwa kushirikiana na
Afisa Utafiti Mifugo anayesimamia.
 Kufanya kazi zozote kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa
na Serikali.
4.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi

5.0 DAKTARI UTAFITI MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY RESEARCH
OFFICER II) – NAFASI 5
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kujifunza na kumudu mbinu na taratibu za utafiti wa afya na maradhi ya mifugo
 Kuweka kumbukumbu za utafiti
 Kusaidia kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
 Kuandaa mapendekezo ya utafiti (“research proposal”) kwa kushirikiana na
Daktari Utafiti Mifugo anayemsimamia.
 Kufanya utafiti chini ya usimamizi wa Daktari Utafiti Mwandamizi
 Kukusanya na kuchambua takwimu za utafiti unaoendelea.
 Kuchapisha taarifa na makala za utafiti
 Kuendesha semina na maonyesho ya ufugaji bora.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (bachelor degree) katika fani ya Sayansi ya
Tiba ya Mifugo (Veterinary Science) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Bodi ya
Madaktari wa Mifugo nchini.
5.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
6.0 FUNDI SANIFU MAABARA MIFUGO DARAJA LA II (VETERINARY
LABORATORY TECHNICIAN II) – NAFASI 8
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kwa kushirikiana na Afisa Mifugo Msaidizi, atafanya uchunguzi wa magonjwa ya
mifugo katika eneo lake.
 Atakusanya sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa maabara.
 Kuwasaidia wataalam kuanda vifaa vya uchunguzi
 Kutunza Usafi wa Maabara na vyombo vilivyomo.
 Kutunza takwimu za uchunguzi
 Atafanya kazi zingine zozote kama atavyopangiwa na mkubwa wake wa kazi
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha sita (VI) waliofuzu mafunzo ya miaka miwili (2)
ya Stashahada katika fani ya Fundi Sanifu Maabara (Mifugo) kutoka Chuo cha
Mifugo (LITI), au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
6.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

7.0 MKUFUNZI MIFUGO DARAJA II (LIVESTOCK TUTOR II) – NAFASI 8
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo.
 Kuandaa mtiririko wa kila somo (Lesson Plan) kwa upande wa nadharia na
vitendo.
 Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendelo ya wanachuo kwa kushirikiana na maofisa mifugo wa wilaya,
viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo.
 Kufanya kazinyingine zozote za fani yake atakavyopangiwa na mkuu wake wa
kazi.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya Sayansi ya Mifugo
kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na
Serikali.
7.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
8.0 MKUFUNZI WA MIFUGO MSAIDIZI (ASSISTANT LIVESTOCK TUTOR) –
NAFASI 7
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa mtiririko (Lesson Plan) wa masomo
 Kufundisha kozi ya astashahada ya mifugo na wafugaji.
 Kusimamia masomo ya vitendo chini ya usimamizi wa Mkufunzi Mkuu wa somo
 Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo
 Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo
 Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo (dairy, poultry, maabara, museum,
nk).
 Kufanya kazi nyingine kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (VI) waliofuzu mafunzo ya Stashahada ya
mifugo kutoka MATI/LITI au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
8.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

9.0 DAKTARI MIFUGO MKUFUNZI DARAJA LA II (VETERINARY TUTOR II) –
NAFASI 3
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
 Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadharia na
vitendo
 Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo.
 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao.
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na madaktari /maofisa mifugo
wa wilaya, wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practicals).
 Kufanya kazi nyingine zozote kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Tiba ya Mifugo kutoka Chuo
Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Wawe wamesajiliwa na Bodi ya Madaktari Tanzania.
9.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi
10.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 3
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusaidia kuunda boti za uvuvi
 Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
 Kufanya matengenezo ya boti.
 Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
 Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye stashahada ya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo
kingine kinachotambuliwa na Serikali.
10.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi

11.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 11
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
 Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
 Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
 Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
 Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu
za umwagiliaji,
 Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
 Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji,
 Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
 Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
 Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
 Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka
Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
11.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E kwa
mwezi.
12.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 50
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
 Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
 Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
 Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C”
ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi
Daraja la II (Trade test II).

12.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS. A kwa mwezi.
13.0 AFISA VIPIMO DARAJA LA II- NAFASI 1
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
 Kutunza na kuhifadhi vifaa vya kitaalamu vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
 Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
 Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya vipimo;
 Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na wateja;
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada ya kwanza katika fani ya Legal Metrology au Legal
and Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
 Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sanyansi ambao wamepata
crash programme in Legal and Industrial Metrology isiyopungua miezi minne (4)
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
 Kuajiriwa mwenye Shahada katika fani ya Uhandisi / Sayansi ambao wamehitimu
Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya Vipimo kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
 Kuajiriwa mwenye Stashahada ya juu katika fani ya Legal Metrology / Legal and
Industrial Metrology kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani WMAS 3 kwa mwezi
14.0 MKUFUNZI DARAJA LA II –MHANDISI MAJI (WATER TECHNOLOGY) –
(NAFASI 11) (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto. Mhandisi huyu atafanya kazi ya kufundisha somo la Uhandisi
wa Maji katika vyuo vya maendeleo ya Jamii Tanzania Bara
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la Uhandisi maji katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kujifunzia na kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti

 Kutoa Ushauri wa kitaalam kuhusu somo la uhandisi maji.
 Kutunga na kusahihisha Mitihani ya wanachuo.
 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayoizunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya Uhandisi Maji (Water Technology) kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
14.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
15.0 MKUFUNZI DARAJA LA II –MHANDISI MITAMBO (METAL TECHNOLOGY) –
(NAFASI 2) (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
Ufundi Mitambo katika vyuo vya maendeleo ya Jamii Tanzania Bara
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la ufundi mitambo katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kujifunzia na kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu somo la uhandisi maji.
 Kutunga na kusahihisha Mitihani ya wanachuo.
 Kufanya utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
 katika jamii inayozunguka chuo
 Kutoa ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya Uhandisi Mitambo (Metal Technology) kutoka
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
15.3 MSHAHARA

 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
16.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- UUNGAJI VYUMA (MECHANICAL ENGINEER)-
(NAFASI 24) (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
Uungaji vyuma katika vyuo vya maendeleo ya Wananchi Tanzania Bara
16.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la uungaji vyuma katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani
 Kufanya Utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayozunguka chuo
 Kutoa ushauri juu ya kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
16.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya Uungaji vyuma (Mechanical Engeneering)
kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
16.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
17.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- MHANDISI UJENZI (CIVIL ENGINEER)-(NAFASI
25) (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia
Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
Ujenzi katika vyuo (24) vya Maendeleo ya Wananchi na Chuo cha Maendeleo
ya Jamii Misungwi

17.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la ujenzi katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani
 Kufanya Utafiti utakaosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayozunguka chuo
 Kutoa ushauri juu ya kuboresha taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya uhandisi majengo(Civil Engeneering) kutoka
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali
17.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
18.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- COMPUTER SCIENCE (NAFASI 5)
(LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
computer na electronics (Computer Application) katika Vyuo vya Maendeleo ya
Wananchi Tanzania Bara.
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la computer na electronics katika Vyuo vya Maendeleo ya
wananchi.
 Kutayarisha mpango kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani

 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayozunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya computer science kutoka katika vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
18.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
19.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- ELECTRICAL ENGINEER - (NAFASI 20)
(LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto. Wakufunzi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
Umeme wa majumbani (Electrical installation) katika vyuo vya maendeleo ya
Jamii Tanzania Bara
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la umeme wa majumbani katika vyuo vya maendeleo ya
wananchi.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani
 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayoizunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika fani ya Electrical Engineering kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali. 

19.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
20.0 MKUFUNZI DARAJA LA II- KILIMO (AGRICULTURAL OFFICER )- (NAFASI
10) (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto. Wakufunzi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la
kilimo (Agriculture) katika Vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania Bara
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la kilimo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani
 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayoizunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/
stashahada ya juu katika somo la kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na
Serikali.
20.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
21.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA II – HOME ECONOMICS/ DOMESTIC
SCIENCE (LINARUDIWA)
(NAFASI 9)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto. Wakufunzi wasaidizi hawa watafanya kazi ya kufundisha
somo la ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe katika vyuo vya maendeleo
ya wananchi Tanzania Bara

21.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha masomo ya ushonaji, ufumaji, kudarizi na upishi na lishe katika vyuo
vya maendeleo ya wananchi.
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam
 Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
 Kutunga na kusahihisha Mitihani
 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
katika jamii inayoizunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya
chuo
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya stashahada ya
ufundi katika fani zaushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe kutoka vyuo vya
ufundi vinanvyotambuliwa na Serikali.
21.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
22.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) –
NAFASI 45 (LINARUDIWA)
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
 Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
 Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi na wageni, tarehe za
vikao, safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa.
 Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
 Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
 Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo,
na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.

 Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na
Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya
Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
katika programu za'' Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher''
22.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
23.0 MPISHI DARAJA LA II (COOK II ) NAFASI – 12 (LINARUDIWA)
 Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia
Wazee na Watoto Wapishi hawa watafanya kazi ya kuwapikia wanachuo katika
vyuo vya maendeleo ya wananchi
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa chakula cha wanachuo kulingana na Menyu na idadi ya wanachuo
 Kupika chakula cha wanachuo
 Kutoa ushauri kwa uongozi wa chuo kuhusu chakula cha wanachuo.
 Kusimamia jiko.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya cheti
yasiyopungua mwaka mmoja katika moja ya fani ya “food Production”
yatolewayo na vyuo vya Forodhani (Dar es Salaam),Masoka (Moshi), Arusha
Hotel, Y.M.C.A (Moshi), VETA (mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) kutoka
vyuo vinavyotambuliwa na serikali na wenye uzoefu wa kazi kwa muda
usiopungua miaka mitatu.
23.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGSC kwa mwezi.
24.0 MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 38
24.1 MAJUKUMU YA KAZI

 Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina
hati ya idhini.
 Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
 Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
 Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho
wa saa za kazi.
 Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya
kufanya hivyo.
 Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile,
moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile,
moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
 Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT
au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
24.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
25.0 MSAIDIZI WA MAKTABA (LIBRARY ASSISTANT) - NAFASI 8
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandikisha wasomaji.
 Kupanga vitabu katika rafu (Shelves)
 Kuazimisha na kupokea vitabu vinavyoazimwa.
 Kukarabati vitabu vilivyochakaa,
 Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kituo.
25.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa waliohitimu cheti cha Mtihani wa Taifa wa kidato cha IV ambao
wamefaulu mafunzo ya Wasaidizi wa Maktaba (National Library Assistants
Certificate Course) yatolewayo na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania au
wenye cheti kinacholingana na hicho.
25.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS. B kwa mwezi.
26.0 DEREVA MITAMBO DARAJA LA II – NAFASI 1

26.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa Dereva Mitambo mwenye uzoefu.
26.2 2.2. SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye cheti cha kidato cha IV ambao wana leseni Daraja la „‟G‟‟ ya
kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo hiyo,
wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua miezi mitatu (3)
bila kusababisha ajali.
26.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara
TGOS A kwa mwezi.
27.0 MPIMA ARDHI DARAJA LA II (LAND SURVEYOR GRADE II) – NAFASI 15
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Sehemu ya Upimaji Milki (Cadastral Survey)
 Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye kompyuta.
Sehemu ya Topographic na Geodetic Surveys
 Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye
kompyuta.
 Sehemu ya Ramani
 Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment);
 Kuandaa vikosi kwa ajili ya kuhuisha ramani (map revision)
 Kutunza kumbukumbu za picha za anga.Sehemu ya Hydrographic Surveys
 -Kusimamia na kuchukua vipimo vya tide gauges.
 Halmashauri za Serikali za Mitaa :
 Kufanya kazi za nje ya Ofisi (field survey operations) chini ya usimamizi wa
mpima aliyesajiliwa.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Stastahada ya juu/Shahada kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi katika
fani ya Upimaji Ardhi au Taasisi yoyote inayotambuliwa na National Council of
Professional Surveyors (NCPS). Au
 Kuajiriwa wenye cheti cha East African Land Survey (EALSC) au National
Council of Professional Surveyors Certificate (NCPSC) katika fani ya upimaji
ardhi.
3.1 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi

28.0 MTEKINOLOJIA WA SAMAKI MSAIDIZI DARAJA LA II (ASSISTANT FISH
TECHNOLOGIST II) – NAFASI 1
3.2MAJUKUMU YA KAZI
 Kutengeneza na kuhifadhi samaki
3.3SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita waliofuzu mafunzo ya miaka miwili
ya uhifadhi na biashara ya samaki (Fish Processing and Marketing) kutoka chuo
cha maendeleo ya uvuvi Mbegani au chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
3.4 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B kwa mwezi
29.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT) – NAFASI
2
29.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira
hatarishi
 Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira
hatarishi
 Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na
watu wenye dhiki
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na
elimu, uzoefu na ujuzi wake
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita na wenye cheti cha mafunzo ya
mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
29.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C Kwa
mwezi.
30.0 MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS ATTENDANT)
– NAFASI 1
30.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kusafisha Vyombo vya kupikia.

 Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
 Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
 Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.
 Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
 Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne.
30.3 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS A kwa mwezi.
31.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II – NAFASI 25
31.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
 Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
 Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
 Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
 Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
 Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
 Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
 Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
 Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
 Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao
mengine,
 Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,
 Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
 Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
 Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla
ya kupitishwa,
 Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
 Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
 Kufanya utafiti mdogo mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya
kilimo cha umwagiliaji,
 Kufanya utafiti wa udongo,
 Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
 Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
 Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi
maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.

31.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor degree) ya kilimo au shahada ya
sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo
Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
31.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa
mwezi.
32.0 FUNDISANIFU MSAIDIZI (WELDING AND FABRICATION) - NAFASI 2
(LINARUDIWA)
32.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi za kutengeneza vifaa na mitambo mbalimbali katika eneo lake.
 Kufanya ukarabati (repair) wa vifaa, pamoja na mitambo mbalimbali.
 Kutunza na kuweka kumbukumbu katika karakana.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua
ya II katika fani ya „Welding and Fabrication‟ kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali.
32.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
33.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UMEME) - NAFASI 5 (LINARUDIWA)
33.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi za matengenezo ya vifaa na mitambo ya umeme.
 Kufunga mashine na vifaa vya umeme katika Eneo Lake.
 Kutunza na kuweka kumbukumbu katika karakana.
 Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu
mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya Umeme kutoka katika Chuo
kinachotambulika na Serikali.
Au

 Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua
ya II katika fani ya Umeme kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na
Serikali.
33.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
34.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 25
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara
ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu
Tawala Mkoa wa Mtwara, na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Chamwino, Tunduru
na Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania.
34.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
 Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
 Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
 Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
 Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na
NBAA
35.0 MHANDISI DARAJA LA II - MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) – (NAFASI
10)
 Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga na Geita, Mkurugenzi Halmashauri ya manispaa ya Temeke,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya za Rungwe, Busega na Chamwino.
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Ujenzi na Usimamizi wa Vituo vya Hali ya Hewa, Vituo vya Upimaji wingi wa Maji
mitoni (Discharge Measurements) na Uchukuaji wa sampuli za mchanga
unaosafirishwa kwenye mito (sedment sampling) na kuzitafsiri.
 Ukusanyaji wa takwimu kwenye vituo vya hali ya hewa na upimaji wa wingi wa
maji mitoni na kuzitafsri takwimu hizo.
 Kuandaa na kutayarisha Taarifa ya robo, nusu na mwaka mzima katika sehemu
ya Haidrologia.
 Kutayarisha kielelezo cha mtiririko wa maji ( Rating Curve Eqution )
35.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
35.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
36.0 FUNDISANIFU DARAJA LA II (UJENZI) - (CIVIL TECHNICIAN GRADE II) –
NAFASI 25
 Nafasi hizi ni kwa kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Morogoro,
Mkurugerugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mpanda, Mbulu, Meatu,
Ilemela, Sengerema, Tunduru, Bukoba Ngorongoro na Kyela na Mkurugenzi
Halmashauri ya Mji Njombe.
36.1 MAJUKUMU YA KAZI
Mafundi sanifu watapangiwa kazi na Mamlaka zinazohusika katika fani zao
kutegemea cheo, ujuzi, uzoefu na uwezo wao pamoja na utendaji mzuri wa kazi
kama ifuatavyo:-
 Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga
mabomba;
 Kuchonga vifaa vya nyumba za Serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”;
 Kufanya kazi za upimaji (survey) wa barabara, majengo na mifereji kama
atakavyoelekezwa;
 Kuwapangia kazi Mafundi sanifu wasaidizi na kuhakikisha wanamaliza kama
ilivyopangwa.
36.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
 Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.
 Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo
vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,
 Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali,
 Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
36.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi

37.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT TECHNICIAN - WATER) NAFASI
5 (LINARUDIWA)
37.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupima uwingi wa maji mtoni
 Kusoma kituo cha hali ya hewa
 Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
37.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya
mwaka mmoja kutoka kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III katika
fani ya maji.
37.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
38.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - HAIDROJIOLOJIA (TECHNICIAN GRADE II -
HYDROGEOLOGIST) – NAFASI 1 (LINARUDIWA)
38.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuhakiki nuwezo wa kisima kutoa maji (Pump test)
 Kuchora ramani za eawali za kiufundi
 Kuhifadhi taarifa za kikazi (Field Data) zipatikanazo wakati wa utafiti wa maji
chini ya ardhi.
38.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Kawaida ya Rasilimali za Maji
na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
38.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
39.0 MKUFUNZI DARAJA LA II (TUTOR II) - JIOLOJIA – NAFASI 1
39.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
 Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadhari na vitendo
 Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na
vitendo

 Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa
kujifunza
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote
kinachohusika na kutunza alama zao
 Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na wahandisi wa
uchenjuaji/jiologia na wahandisi migodi wa viwandani wa mafunzo kwa vitendo
(Field Practicals)
 Kufanya kazi nyingine kulingana na kiwango cha elimu na fani yake kadri
atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi
39.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na Shahada ya Sayansi katika fani ya jiolojia (pamoja na fani za jiofizikia au
jiokemia) au sifa nyingine zinazolingana na hizo kutoka vyou vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali.
39.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa
mwezi.
40.0 OPERATA WA KOMPYUTA DARAJA LA II (COMPUTER OPERATOR) -
NAFASI 1
40.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi za kompyuta/programu zenye mifumo migumu kwa usimamizi wa
wastani wa Maopereta wa Kompyuta Waandamizi
 Kurekebisha mpango wa kazi katika chumba cha kompyuta
 Kutunza vitabu vya matumizi ya kila siku ya kompyuta
 Kuhifadhi data zote zinazoingizwa katika kompyuta
 Kuchapa taarifa za mwisho
40.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye stashahada ya masomo ya kompyuta kutoka kwenye
Taasisi/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
40.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa
mwezi.
41.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - (TECHNICIAN GRADE II - PLUMBING) –
NAFASI 5

41.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi za ufundi bomba atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
41.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
 Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka
Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya fundi bomba (Plumbing)
 Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi bomba ya miaka mitatu
kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani
za ufundi
 Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi
kinachotambuliwa na Serikali
 Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi bomba kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
41.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
42.0 FUNDI SANIFU MAABARA – (WATER LABORATORY TECHNICIAN)
DARAJA II – NAFASI 7.
42.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kumsaidia Fundi Sanifu Daraja I katika kazi ili kupata uzoefu
 Kutafsiri maelezo ya matumizi ya madawa mbalimbali kwa kwa ajili ya kazi
mbalimbali za maabara
 Kusimamia uchukuaji wa sampuli za maji na udongo kwa ajili ya upimaji
 Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vya maabara ya kawaida na ya
dharura yanapohitajika;
 Kufanya upimaji wa maji na udongo wa maeneo ya miradi na kuandaa
maelekezo ya matibabu yanayohitajika.
 Kusimamia ukusanyaji wa takwimu za hali ya maji na udongo zinazohitajika
kwenye maeneo ya miradi
 Kuwaongoza mafundi sanifu wasaidzi kutekeleza kazi zao
 Kutoa taarifa za hali ya maji na udongo wa maeneo ya miradi kwa Mhandisi.
42.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe na Cheti cha Stashahada ya Maji (Water Laboratory) toka Chuo cha Maji au Chuo
chochote kinachotambuliwa na Serikali.
42.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

43.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) –
NAFASI 7
43.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
 Kutunza takwimu za maji
 Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye
michoro
 Kuchora hydrograph za maji
 Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji „cable way post”
 Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
 Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
 Kufundisha wasoma vipimo
43.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao
wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye
ujuzi wa kutumia kompyuta.
43.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
44.0 FUNDI SANIFU – (WATER WORKS TECHNICIAN) DARAJA II – NAFASI 8
(LINARUDIWA)
 Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
44.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kumsaidia Fundi Sanifu Daraja I katika kazi ili kuapata uzoefu wa;
 Kutafsiri ramani za ujenzi wa miundombinu ya maji au ya ufungaji wa mitambo ya
miradi ya maji
 Kujenga miundombinu ya aina mbalimbali au kufunga mitambo ya miradi ya maji
na usafi wa mazingira;
 Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa miundo mbinu
kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa dharura;
 Kusimamia ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za uendeshaji na matengenezo ya
miundo mbinu au mitambo ya miradi ya maji;
 Kuwaongoza mafundi sanifu wasaidizi kutekeleza kazi zao
 Kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa Mhandisi
44.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Awe na Cheti cha Stashahada ya Maji (Water Works Technician) toka Chuo cha Maji au
Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
44.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
45.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI BOMBA) - (ASSISTANT WATER WORKS
TECHNICIAN PLUMBING) – NAFASI - 3 (LINARUDIWA)
 Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
45.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
 Kufunga mitandao ya bomba za aina mbalimbali ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira;
 Kufanya usafi na ukaguzi wa mitandao ya bomba ya miradi ya maji na usafi wa
mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
 Kuwezesha uzalishaji na usambazaji wa maji na utoaji wa majitaka kwa kupitia
mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira.
 Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa mitandao ya
bomba kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa dharura.
 Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kumsaidia Fundi sanifu kazi za kiufundi.
45.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plumbing).
45.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
46.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT TECHNICIAN
GEOMETRIC) – NAFASI 23 (LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
46.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;

 Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za
kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya
maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
 Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya
maji na usafi wa mazingira;
 Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za
usanifu wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya
miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya
kuwezesha usanifu wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
46.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).
46.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
47.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 30
(LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
47.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
 Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
 Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
 Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
 Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
47.2 SIFA ZA MWOMBAJI

 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo ya Maji (Pampu).
47.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
48.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 12
(LINARUDIWA)Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
48.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
 Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi
ya maji na usafi wa mazingira;
 Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na
usafi wa mazingira;
 Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine vya umeme na
miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu
na kuzuia uharibifu;
 Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa
umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na
inapohitajika kwa dharura.
 Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
48.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
48.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
49.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 4
(LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

49.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
 Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
 Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
 Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
 Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
 Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
 Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
49.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.
49.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
50.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI UJENZI (ASSISTANT TECHNICIAN - CIVIL) –
NAFASI 31 (LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
50.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
 Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
 Kufanya kazi za upimaji (Survey) wa barabara, majengo na mifereji kama
atakavyoelekezwa,
50.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa Ujenzi (Civil Technician ) kutoka katika chuo
kinachotambuliwa na Serikali,
 Au
 Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II
(Civil Technician) kutoka chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi Ujenzi. 

50.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
.
51.0 MKUFUNZI MSAIDIZI (ASSISTANT TUTOR) - NAFASI 4
51.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuandaa mtiririko (leson plan) wa somo
 Kufundisha kozi ya astashahada ya uchenjuaji wa madini, jiolojia na utafutaji wa madini
na uhandisi migodi,
 Kusimamia masomo ya vitendo chini ya mkufunzi mkuu,
 Kuandaa na kupanga vifaa kwaajili ya masomo ya vitendo,
 Kuwapima wanachuo wakati wa masomo ya vitendo,
 Kufanya kazi nyingine kulingana na kiwango cha elimu na fani yake kadiri
atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
51.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Awe amehitimu kidato cha nne (IV) au sita (VI) waliofaulu mafunzo ya Stashahada ya
Uhandisi wa Uchenjuaji Madini, Jiolojia au Uhandisi Migodi kutoka chuo
kinachotambuliwa na Serikali.
51.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D Kwa mwezi.
52.0 MHANDISI MIGODI (MKUFUNZI) II TGS E NAFASI 2
52.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha somo la Uhandisi Migodi
 Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
 Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
 Kutunza vifaa vya kujifunzia na kufundishia
 Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
 Kutoa Ushauri wa kitaalam kuhusu somo la uhandisi Migodi.
 Kutunga na kusahihisha Mitihani ya wanachuo.
 Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali katika
jamii inayoizunguka chuo
 Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni.
52.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Shahada/Stashahada yajuu ya Uhandisi katika fani ya Sayansi ya Uhandisi wa Migodi
(Mining Engineer) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

52.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
53.0 MHANDISI NISHATI II NAFASI 5
53.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuratibu miradi ya nishati katika ngazi zote,
 Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali na matokeo ya uvumbuzi na utafiti katika
fani zao,
 Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi bora ya nishati kutokana na maendeleo ya
teknolojia,
 Kufanya ukaguzi wa shughuri za nishati ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora
wa huduma za nishati zitolewazo, uingizaji wa petrol na utunzaji wa nishati,
 Kusimamia utendaji wa kazi wa wahandisi nishati waliopo chini yake.
53.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi wa Nishati (Energy Engineer) kutoka vyuo
vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
53.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
54.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1 (LINARUDIWA)
54.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na
kuzifungasha.
54.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au
mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
54.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa
mwezi.
55.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 1 (LINARUDIWA)
55.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
 Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.

 Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
 Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
 Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
 Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au
wamepata idhini ya maafisa husika.
 Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
 Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
 Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa
kwenda nje.
55.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
55.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
56.0 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - (GARDNER II) NAFASI 3 (LINARUDIWA)
56.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kupanda maua katika maeneo yanayohusika.
 Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji.
 Kupanda mboga, matunda katika bustani.
 Kupalilia mazao katika bustani.
 Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.
56.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Cheti katika fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na
upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au
Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda
usiopungua miaka mitatu.
56.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa
mwezi.
57.0 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II)
– NAFASI 15 (LINARUDIWA)
57.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na
Mafunzo

 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa
vyama na vilabu vya michezo
 Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
57.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo
(Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
57.3 MSHAHARA
 Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
58.0 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)
 Baraza la Sanaa la Taifa ni shirika la Umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na.
23 ya mwaka 1984. (Sheria ya kuunda upya Baraza la Sanaa la Taifa kwa
kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa na Baraza la Muziki la Taifa na kufuta
Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1974 na Sheria ya Baraza la
Muziki la Taifa ya mwaka 1974 na kuweka utaratibu kuhusiana na mambo hayo.
Kazi za Baraza la Sanaa la Taifa ni Kufufua, kukuza na kuendeleza kazi za
sanaa ikiwa ni pamoja na Uhamasishaji, Usimamizi, Uimarishaji, Uratibu, Utafiti,
na Ushauri wa kazi mbalimbali za Sanaa.
58.1 MKURUGENZI WA UTAFITI NA UKUZAJI WA STADI ZA WASANII – NAFASI
1 (LINARUDIWA)
58.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
 Kuongoza Idara ya Utafiti na ukuzaji wa stadi za Sanaa.
 Kuandaa mpango wa Utafiti na kusimamia utekelezaji.
 Kuandaa mpango wa kukuza stadi za wasanii na kusimamia utekelezaji.
 Kuwasiliana na watafiti mbalimbali na kushirikiana nao.
 Kuandaa na kusimamia makubaliano na watafiti wanaojiajiri kwa muda kufanya
tafiti maalum
 Kubaini na kuteua wawezeshaji wa ukuzaji wa stadi za wasanii.
 Kusimamia uchapishaji wa majarida na vitabu vya Baraza.
58.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
 Kuajiriwa wenye Shahada ya Uzamili katika fani za Sanaa na Utafiti kutoka
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
 Uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) ambapo miaka mitano (5) kati ya
hiyo ikiwa ni kwenye nafasi ya uongozi katika idara mbalimbali zilizo chini ya
taasisi za umma.

58.1.3 MSHAHARA
 Mshahara PGSS 14
X. M. DAUDI
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA
============

Avoid scams : NEVER pay to have your CV / Application pushed forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a SCAM.

Share :

Facebook Twitter Google+
2 Comment "NAFASI 632 ZA AJIRA SERIKALINI"

jaman kuna awamu ingine au ndio mwaka ushafungwa? maana kilimo zipo 35 tuu mh!

Back To Top