NAFASI 22 ZA AJIRA SERIKALINI ( HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA)

HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA
(BARUA ZOTE ZIANDIKWE KUPITIA KWA MKURUGANZI MTENDAJI)
Kumb. Na. L.10/7/26
Tarehe: 03/02/2016

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imepokea kibali cha ajira kumb.Na. CB.170/370/01/D/117 cha tarehe 06/01/2016 kutoka kwa katibu Mkuu Ofici ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Hivyo, natangaza nafasi za kazi Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi zifuatazo:-

1. Katibu Mahsusi Daraja la III-Nafasi 3

Sifa

Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne (IV), waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kuaulu mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na kupata cheti katika program za windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
Majukumu
Katibu Mahususi Daraja III atapangiwa kufanya kazi katika “typing Pool” au chini ya katibu Mahususi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye Ofisi ya Mkuu wa sehemu au Kitengo.

• Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
• Kusaidia kupokea wageni, kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
• Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika Ofisi anayofanyia kazi, na kumuarifu mkuu wake wakati unaohitajika.
• Kusidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote kinachohitajika katika shughuli za kikazi hapo ofisini.
• Lisaodia kufikisha maeleo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumuarifu kunusu taarifa zozote anazokua amepewa na wasaidizi hao.
• Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

Ngazi ya Mshahara

Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mishahara Serikalini yaani TGS B
=========

2. Mtendaji wa Kijiji Daraja la III – Nafasi 19

Sifa

Mwenye Elimu ya kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/cheti katika moja ya fani zifuatazo:- utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Sanaa Kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu

• Afisa masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
• Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
• Kuratibuna kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kijiji.
• Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
• Kutafisiri na kusimamia Sera, sheria na Taratibu.
• Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ay kuondia njaa, umaskini na kuongeza uzalishsji mali.
• Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaaluma katika Kijiji.
• Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Vijiji.

Ngazi ya Mshahara

Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mishahara Serikalini yaani TGS B
Masharti ya Jumla
• Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya wilaya ya Mwanga.
• Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa la jinai au kufungwa jela.
• Maombi yote, waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V).
• Maombi yote ya waombaji yaambaane na nakala za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu kidato cha (IV au VI), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (passport size) na iandikwe jina nyuma.
• “Testimonials, provisional Results, statement of results” hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV and FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
• Waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kama wanakibali cha katibu mkuu kiongozi.
• Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika TCU na NECTA na taarifa ya uhakika iambatanishwe kwenye maombi.
• Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
• Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 17/02/2016 saa 9:30 alasiri
• Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashuri ya Wilaya ya Mwanga
S.L.P 176
MWANGA

Jamhuri D. Wiliam
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashuri ya Wilaya
MWANGA

Source: Mwananchi 10th February, 2016
============

Avoid scams : NEVER pay to have your CV / Application pushed forward. Any job vacancy requesting payment for any reason is a SCAM.

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment "NAFASI 22 ZA AJIRA SERIKALINI ( HALMASHAURI YA WILAYA YA MWANGA)"

Back To Top